Let’s talk

The Tanzania Scouts Association is the leading movement for young people in the country, boasting a minimum of 3,632 members. The association continues to engage with various programs and activities across schools and universities nationwide.


Register Now!!

About Us

Tanzania Scouts Association

Tanzania Scouts Association (TSA) is a registered member of the World Organization of the Scout Movement (WOSM).  It is a voluntary, non-political educational movement for young people open to all without distinction of origin, race or creed in accordance with the purpose, principles, and method conceived by its Founder.  Scouting is education for life aimed at helping young people learn skills and values to become responsible active citizens. 

Uongozi wa Bodi ya Chama cha Skauti Tanzania, kupitia kikao chake kilichofanyika tarehe 24/04/2025, umeidhinisha kuanza rasmi kwa mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wa Bodi ya Skauti Taifa.


Kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania (Toleo la 2024), Ibara ya 21, uchaguzi huu unazingatia mwongozo uliowekwa katika Sera, Mwongozo na Sheria za Skauti (S.M.S/P.O.R)


1. Nafasi Zinazogombewa:

Jumla ya nafasi sita (6) za Wajumbe wa kuchaguliwa wa Bodi ya Skauti Taifa zitajazwa.

 Mgawanyo wa nafasi ni kama ifuatavyo:

  • Wawakilishi wawili (2) kutoka Tanzania Bara
  • Wawakilishi wawili (2) kutoka Zanzibar
  • Wawakilishi wawili (2) kutoka kwa Skauta Wazoefu  katika Mafunzo (Mkufunzi) au Programu ya Vijana

 

2. Taratibu za Uchaguzi:

  • Mgombea atatakiwa kupitia mchakato wa uchunguzi wa maadili, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha ripoti ya polisi (Police Clearance Report) kuthibitisha kutokuwa na historia ya uhalifu.
  • Mgombea atatakiwa kujaza fomu inayopatikana kwenye tovuti ya Skauti www.tanzaniascouts.or.tz 
  • Uchaguzi utafanyika katika Mkutano Mkuu, baada ya mchujo wa awali.
  • Gharama ya fomu ya kugombea ni Tsh 100,000/= (nonrefundable), inayopaswa kulipwa kupitia akaunti ifuatayo:

  • Jina la Akaunti: Tanzania Scouts Association
    Akaunti Na.: 20910006475
    Benki: NMB Bank


3. Sifa za Mgombea:

Awe Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwenye Umri usiopungua miaka 26 na usiozidi miaka 70

Awe na uzoefu/ujuzi katika mojawapo ya nyanja zifuatazo: utawala, fedha, sheria, maendeleo ya jamii, elimu, au taaluma nyingine.

Awe na uadilifu, uwajibikaji, na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika vikao vya Bodi

Asiwe amewahi kuthibitika kufanya kosa la kiadili au la kisheria

Awe tayari kujitolea kwa moyo wa Skauti

Akubaliane na misingi, kanuni na maadili ya Skauti


4. Jinsi ya Kuwasilisha Maombi:

Waombaji wanapaswa kuwasilisha:

  • Taarifa ya polisi (Police clearance form)
  • Nakala ya wasifu binafsi (CV)
  • Nakala ya kitambulisho cha NIDA
  • Nakala ya vyeti vinavyoonesha uzoefu na sifa stahiki
  • Nakala ya risiti ya malipo ya fomu kutoka benki
  • Nakala ya risiti ya ada kwa miaka 2024/2025 (kwa Skauta)
  • Barua ya Motisha (Motivation letter)


5. Tarehe Muhimu:

Mwisho wa kupokea maombi: Tarehe 31 Mei 2025, saa 10:30 jioni kwa njia ya mtandao tu.

Anuani ya kuwasilisha maombi: info@tanzaniascouts.or.tz

Tarehe ya uchaguzi: Tarehe 03 Julai 2025


6. Maelekezo Zaidi:

Maelezo mengine ya uchaguzi na mchakato mzima yatatolewa baadaye kupitia njia rasmi za mawasiliano za Chama.

Imetolewa na:

 

 Eline Kitaly
Kamishna Mtendaji



 

The Story of Scouting


There are over 50 million Scouts, both male and female, in more than 200 countries and territories.

What are the Scout Laws?

A Scout's honour represents trustworthiness and integrity as a commitment to responsible citizenship, embodying respect, loyalty, and service to God, country, family, and others, which strengthens community bonds and mutual support.

Scouts Historical Highlights


Recurring events like World Scout Jamborees, Moots, and World Scout Conferences are only referenced by their initial occurrence.

Mafunzo ya Awali ya Uongozi


Mafunzo ya Awali ya Uongozi (PTC) ya kwanza kwa mwaka 2025 yalifanyika Jijini Dodoma mwezi Januari.

Ndoto ya Kijana

Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023 wakimsaidia kijana Skauti (W) Kigamboni ambaye aliyekuwa na ndoto ya kuushika Mwenge huo.

Malengo Endelevu ya Dunia

Vijana wa Skauti wakiwa katika picha wakati wa moja ya mafunzo yao.

 

OUR ACHIEVEMENTS

What we’ve done so far

We have implemented several programs that include various community projects, such as Messenger of Peace, Growth, Mental Health, Food for Life, Plastic Tide Turner, Anti-Drugs initiatives, Reproductive Health and Youth for Peace Agenda.

Additionally, we collaborate with various institutions, both governmental and non-governmental organizations, to enhance the impact of our efforts.

3632 +

Total Members

G4057

Total Scout Groups

4.000

Total Project on sites

12.000 +

Total Partners

 

CHAMA CHA SKAUTI KIMEFANYA TATHIMINI YA USALAMA DHIDI YA MADHARA (SfH)


Chama cha Skauti Tanzania kimeingia katika historia ya Vyama vya Skauti Vitano (5) Kanda ya Afrika vilivyoteuliwa kufanyiwa tathimini ya Usalama dhidi ya Madhara (SfH) ulioendeshwa na WSB kanda ya Afrika yenye Makao Makuu yake Nairobi, Kenya. Tathimini hiyo imefanyika Makao Makuu ya Skauti, Upanga Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 22 Juni, 2025 ikisimamiwa Erick Mwenda, LT (Mtathimini) na Mostaff Moteswana, LT (Mkuu wa Idara ya Usalama dhidi ya Madhara (SfH) Kanda ya Afrika.


Tathimini hii ilikuwa na lengo la kuhakikisha Chama cha Skauti Tanzania kinakidhi vigezo vya ulinzi na usalama wa mtoto, kijana na Skauti kwa ujumla.

Habari njema ni TSA imezingatia vigezo na kupita katika tathimini ya Usalama dhidi ya Madhara (SfH)



OUR MISSION

The mission

The Tanzania Scouts Association (TSA) is on a mission to foster the education of young people through a value system rooted in the Scout Promise and Law. This initiative aims to cultivate a better world by enabling individuals to realize their full potential while playing a constructive role in society.


By engaging youth throughout their formative years in a non-formal educational process, TSA employs specific methods that position each individual as the key agent in their own development. The goal is to nurture self-reliance, support, responsibility, and commitment, helping young people establish a value system grounded in spiritual, social, and personal principles as outlined in the Scout Promise and Law.

Our partners and collaborators

Plastic Tide Turner Training

On January 30-31, 2025, a successful Plastic Tide Turner training took place in Dar es Salaam, involving 30 young participants and 9 adults from Dar es Salaam, Tanga, and Zanzibar, focused on innovative plastic waste management solutions. The event included hands-on activities, discussions, and workshops aimed at empowering local communities to address plastic pollution.


Officially opened by Tanzania Scouts Association Chief Commissioner LT. Abubakari Mtitu and concluded by National Board Member Mr. Juma Dossa, the training emphasized environmental advocacy and was facilitated by Ms. Grace Kamau from the World Scout Bureau.


Local Scouts in Dar Es Salaam organized a community clean-up at Kivukoni Ferries Beach to beautify the area and reinforce environmental principles learned during their training. Scout leaders emphasized the initiative as a way to give back and instill conservation values in youth. The event attracted local residents and environmental enthusiasts, raising awareness about the importance of maintaining clean beaches and the impact of pollution on marine life. This clean-up reflects the Scouts' commitment to positively impacting their community and promoting sustainability for future generations.


Beach Clean-ups - Zanzibar

Volunteers gathered at Kizingo and Forodhani beaches to diligently remove litter, showcasing their commitment to preserving Zanzibar's natural beauty. This clean-up event served as a practical application of the Scouts’ training, highlighting the significance of environmental stewardship and community engagement.

SKAUTI NA ZIMAMOTO KUIMARISHA HUDUMA ZA DHARURA NCHINI

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga, ameshukuru ushirikiano kati ya jeshi hilo na Chama cha Skauti Tanzania, akisistiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano huo. Masunga alitoa kauli hiyo tarehe 15 Aprili 2025 alipotembelewa na Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, Abubakari Mtitu, pamoja na Kamishna Mtendaji Eline Kitaly, katika ofisi zao Dodoma. Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kupitia upya makubaliano ya ushirikiano katika operesheni mbalimbali yaliyoanzishwa miaka mitano iliyopita. Ushirikiano kati ya Jeshi la Zimamoto na Skauti umekuwa na mafanikio makubwa katika utoaji wa elimu ya kinga dhidi ya majanga na kutoa msaada katika maokozi.

(Picha na Jeshi la Zimamoto)

Makubaliano ya Ushirikiano (MoU)

Viongozi wakuu wa Taasisi ya TAKUKURU, ZAECA na SKAUTI (TSA) wakiwa wameonyesha Makubaliano ya Ushirikiano baada ya kusaini nyaraka zinazothibitisha ushirikiano wao.

Makubaliano ya Ushirikiano (MoU)

Viongozi wakuu wa Taasisi ya ZAECA, TAKUKURU, na SKAUTI (TSA) wakiwa wameonyesha Makubaliano ya Ushirikiano baada ya kusaini nyaraka zinazothibitisha ushirikiano wao.

Usalama dhidi ya Madhara (SfH)


Usalama wa washiriki wote ni kipaumbele chetu katika hafla yoyote ya Skauti. Kuhakikisha kwamba watoto na vijana wanakumbatiwa na Usalama na Kinga dhidi ya Madhara ni kiini cha misheni yetu ya Skauti. Ni sera muhimu ya Chama cha Skauti Tanzania (TSA) kuhakikisha kwamba vijana na watu wazima wanalindwa.


Sisi huwa tunalenga kuwahakikishia watu usalama wa kimwili na afya wakati wa shughuli na katika kambi. Ni muhimu sana pia kuwakinga dhidi ya madhara yanayoweza kutokana na wengine au wao wenyewe. Hafla haipaswi kuendelea hadi iwe na mpango thabiti wa Usalama na Kinga dhidi ya Madhara na njia za kuitekeleza.


Watu wazima wote wanaoshiriki wanawajibika kwa usalama wa watoto na vijana wanaoshiriki katika hafla za Kimataifa na za Mikoa. Mwongozo wake (SERA) umeundwa kusaidia waandaaji wa Hafla za Skauti za Kitaifa au za Mikoa, Wilaya na Kundi kuunda mazingira salama kwa washiriki wote na timu ya upangaji, kabla na wakati wa hafla.


Waweza kusoma na kufuata Waraka wa Usalama dhidi ya Madhara wa 2025 hatua kwa hatua ili kuhakikisha muundo thabiti wa Usalama na Kinga dhidi ya Madhara kwa hafla yako.


Nyongeza zina vielelezo na nyenzo za usaidizi ambazo unaweza kutumia kwa hafla yako. Usisite kuwasiliana na Waratibu wa Usalama Dhidi ya Madhara kupitia Huduma ya Usalama na Kinga dhidi ya Madhara kwa msaada. Skauti Njema!


ORODHA YA WARATIBU WA USALAMA DHIDI YA MADHARA (SAFE FROM HARM) WA MIKOA

NA

JINA KAMILI

MKOA

Simu

E-Mail

1

ELEVINA PETER MSOGOYA

KILIMANJARO

0765574218

msogoyaelevina@gmail.com

2

DEOGRATIUS WILIAM KIMARYO

MARA

0762340177

deogratiuswillium1@gmail.com

3

MWAJABU JAFFARY MAKALA

PWANI

0617398827

makalamwajabu@gmail.com

4

WILSON BISWALO GEORGE

SIMIYU

0750822105

wbiswalo1989@gmail.com

5

AMINA ABDALLAH BAKARI

KASKAZINI PEMBA

0714198657

aminabakar016@gmail.com

6

BAHATI SIMON MSISA

TABORA

0629584971

Sluckson71@gmail.com

7

VICTOR NICOLA BAYNI

MANYARA

0620100465

victorbaynit@gmail.com

8

JOHN HARAMELA PABANDI

SHINYANGA

0764485222

haramela.john@gmail.com

9

GRACE JOHN MASSAWE

KATAVI

0758556536

gracemassawe06@gmail.com

10

MAHAMUD MOHAMED SADALA

DAR ES SALAAM

0689152940

mohamedsadallah06@gmail.com

11

MOHAMED NYANGE JUMA

KASKAZINI UNGUJA

0773076945

mohdnyange5@gmail.com

12

FATUMA AYUBU NKUBI

SINGIDA

0753991364

Farajaayubu7@gmail.com

13

ROGERS JOSEPH CHAMANI

TANGA

0713510324

rogerschamani@yahoo.co.uk

14

JENNY JOHN MIHEMBI

DODOMA

0676291133

mihembijenny@gmail.com

15

AGNESS PIUS MWANISENGO

MBEYA

0764316841

Agnespius302@gmail.com

16

JORFAM DAVID DOMONDO

MWANZA

0715365674

domondojoram@gmail.com

17

MERCY JOSEPH KUNAMBI

MOROGORO

0768734975


18

JAZILA MIKIDADI NYAMBI

ARUSHA

0775088591


19

ZAHRA MUSA HASSAN

KUSINI UNGUJA



20

RAMADHANI NDASI

KIGOMA

0712695959


21

SALOME HENRY KAVISHE

RUVUMA

0628163751


22

LUJAINA HAJJ ABDALLAH

MJINI MAGHRIB

0718092069


23

GODRIVER BATHLOMEW BINIGIRI

MTWARA

0655054050


24

ITIKAVU DANIEL KIBIKI 

IRINGA

0753149849


25

CHRISTOPHER BENEDICT KAVINA

GEITA

0759215795

 

26

KIMALI LEMBO DILA

LINDI

0710056265


27

GODFREY MENARD KAYANGE

RUKWA

0623560605


28

ORETA SIMWINGA

SONGWE

0718920904


29

PETER MATHIAS MHEMA

NJOMBE

0754586574


30

JAMES RWENYAGIRA MAIGA

KAGERA

0759446119


31

HAMADI HAMISI ALI

KUSINI PEMBA

0657052473

Toa taarifa dhidi ya Unyanyasaji

Safe From Harm (SfH) ni mkakati maalumu unaolenga kuhakikisha kuwa Skauti wote na vijana wote wanakuwa salama kutokana na aina zote za ukatili au madhara katika shughuli zote za Skauti na nje ya mazingira ya Skauti/jamii. Kila Skauti anawajibu wa kuelimisha jamii na kutoa taarifa kwa mamlaka kuhusu ukatili unaowakabili watoto au Skauti wenzake, popote walipo, bila hofu yoyote.

 

KANUNI ZA MAADILI ZA USALAMA DHIDI YA MADHARA.

(SOMA ELEWA NA USAINI)


 

Usalama dhidi ya Madhara

Toa taarifa kupitia fomu hii maalumu kwa Skauti yoyote au rafiki wa Skauti aliyeko tayari kutoa taarifa kuhusu ukatili au madhara yanayowakabili watu, hasa watoto. Taarifa zitakazotolewa kupitia fomu hii zitatunzwa kwa siri kwa matumizi ya ofisi pekee.


+255 750 391 138

sfh@tanzaniascouts.or.tz

P.O. Box 945, Dar es Salaam, Tanzania

1101 Upanga, Block No. 1078, Malik Road